Rubberband Box Braids( Rasta za Rababendi)

Wiki iliopita niliingia youtube kuangalia style rahisi ya kusuka. Katika pita pita yangu nikaona style ya rasta ambayo unatumia rababendi, nikasema enh style si ndio hii acha nijaribu. Nikaenda dukani, nikanunua rasta na rababendi. Nimerudi nikanza kujisuka. I was very excited yaani. 

Nikajisuka mpaka nikamaliza. Nilitumia about 7 hours.

Nilivyo maliza eh bwana weeeeeeeeeh!!!!!!!!!!😥😥😥😥, niliumwa na kichwa ile mbaya. Ilikuwa Jumamosi usiku sikulala usiku huo kabisa. Nikajipa moyo oh itapungua… Wapi!!!!! Siku ya pili yake nilikuwa hali ile ile na zaidi. Kichwa kinauma mpaka basi, Nikajaribu kuvumilia aaahhhh siku inayofata nikashindwa nikazitolea mbali aiseee. Yaani haya mambo mengi tuwaachie wenye kuyaweza🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣. Huo ndio mwanzo na mwisho wa Rasta za rababendi (Rubberband box braids). 

#hairstyles #boxbraids

Author: Mamu

Leave a Reply

Your e-mail address will not be published. Required fields are marked *